19 Sep 2024 / 87 views
Tetesi za soka Ulaya

Al-Nassr wanamlenga kiungo wa kati wa Manchester City na Croatia Mateo Kovacic, 30, katika dirisha la uhamisho la Januari kwa malipo ya zaidi ya £750,000 kwa wiki.

Mshambulizi wa Liverpool wa Misri Mohamed Salah, 32, ana nia ya kusaini mkataba mpya ili kuongeza muda wake wa kusalia Anfield. (Liverpool Echo),

Liverpool wanapanga kufanya mazungumzo na Salah kuhusu mkataba mpya siku za usoni.

Vinginevyo, Liverpool wanatarajia Salah, mlinzi wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, na kipa wa Brazil Alisson, 31, wote kuhamia Saudi Arabia msimu ujao.

Kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 32, atazingatia ofa za kuondoka Manchester United ikiwa ataambiwa kuwa hana mustakabali Old Trafford.

Manchester United na Newcastle bado wamechanganyikiwa kuhusu usajili wa kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru huku ofa kutoka kwa Galatasaray ikiwa mezani kwa mchezaji huyo wa zamani wa Juventus.